Michuano ya sasa ya Kombe la Maitaifa ya Afrika inamptaia nyota mbabe
na mojawepo wa manusura kutoka enzi iliyotambuliwa kama Ivory Coast, Yaya
Toure, nafasi ya mwisho ya kushinda taji la kimataifa.
Kufuatia kustaafu kwa miamba Didier Drogba na Didier Zokora baada ya
Kombe la Dunia la mwaka jana, Toure, 31, na ndugu yake anayemtangulia,
Kolo wamesalia kama wakongwe wawili kwenye kikosi cha Ivory
Coast ambao walicheza michuano ya kombe la Dunia ya ,mwaka 2006 nchini Brazil.
Ivory Coast wamenusa utukufu wa Afrika baada ya kushindwa
kupitia penalti na Misri jijini Cairo kwenye michuano ya mwaka 2010 na kulazwa kwenye mchezo dhidi ya Zambia mnamo mwaka
2012 kwa karata hiyo hiyo jijini Libreville kwenye juhudi za kuzoa taji
la pili tangu 1992.
Toure ambaye amecheza awamu tatu za Kombe la Dunia anajiandaa
kushiriki dimba la sita la Afrika akijua muda unayoyoma kuongeza medali
ya ushindi na taifa lake baada ya kubobea pakubwa kwenye mchezo wa
kulipwa kwenye vilabu mashuhuri duniani, Barcelona na Manchester City.
Nyota huyo bado anahifadhi makali yake baada ya kutawazwa mshindi wa
taji la mwanasoka bora zaidi Afrika kwa mara nne mtawalia kufanya
historia mbele ya mshambuliaji sugu wa Borrusia Dortmund na Gabon
Pierre-Emerick Aubameyang na kipa wa Lille na Nigeria Vincent Enyeama.
Alikuwa mchezaji pekee wa kutoka bara hili kuingia kwenye orodha ya
2014 FIFA Ballon d’Or inayotambua mchezaji bora duniani ambapo alimaliza
nafasi ya 14 kwenye kura za kutawaza mshindi.
Sifa zake zimesambaa kwa juhudi zake City ambao alifungia magoli 20
na kuwasaidia kunyakua utukufu wa ligi ya Premier ya Uingereza kutoka
kiungo cha kati.
Ameongezea mengine 7 kwenye mechi 18 za ligi ya Premier musimu huu na
licha ya kuonekana kuzembea, amefunika nyasi mingi kushinda mchezaji
yeyote mwingine City muhula huu.
Post a Comment