Mlinzi wa Orlando Pirates Ayanda
Gcaba ameitwa kwenye timu ya taifa ya Afrika Kusini Bafanabafana ili
kuziba nafasi ya Patrick Phungwayo.
Bafanabafana inashiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika michuano itakayoanza Januari 17 mwaka huu.
Phungwayo
ambaye naye ni mchezaji wa Orlando Pirates alilazimika kurudi nyumbani
baada ya kupata majeruhi ambayo hayatamwezesha kuitumikia timu yake ya
taifa.
Kocha wa Bafana bafana Epharaim Shakes Mashaba amesema
amesikitishwa kwa kumkosa Phungwayo lakini ameonyesha kuwa na matumaini
na mbadala wa mchezaji huyo Ayanda Gcaba
wakati huo huo mashabiki
wa timu ya taifa ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo nayo
itashiriki mashindano hayo wamekuwa na matumaini ya timu yao kufanya
vizuri na hata kunyakua kombe hilo.
Post a Comment