Floyd Mayweather ndiye bondia anayelipwa mkwanja mrefu zaidi duniani kwa sasa lakini pia anatajwa kuwa ndiye bondia anayejua kutumia zaidi pesa anayoipata kutokana na nguvu zake.
Kwa mujibu wa jarida la Forbes ni kuwa mwanamasumbwi huyu anaingiza kiasi cha paundi milioni 66.1 kwa mwaka na kumfanya kuwa ndiye bondia anayelipwa zaidi duniani.
hivi karibuni Mayweather
ameposti picha mtandaoni ikimuonesha binafsi akiwa amesimama mbele ya mbele ya magari kadhaa ya kifahari na ndege yake binafsi.
Chini ya picha hiyo mwanamasumbwi huyo aliandika maneno yafuatayo ya kiingereza 'Welcome to my toy world! Who
wants to come out and play?'
Lakini katika kuonesha hali ya kutotishika na kiasi kikubwa cha pesa anachomiliki mwanamamsumbwi huyo, mwanamasumbwi Manny Pacquiao yeye ameposti picha akiwa pembeni ya moto na kuandika sijali kuhusu pesa zake ninachohitaji ni pambano dhidi yake.
Myweather akila raha na mwanawe
Myweather kazini.
Myweather akiwa na binti yake wakiangalia pambano la mpira wa kikapu baina ya LA Lakers na Phoenix
ifuatayo ni orodha ya wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Mchezaji | Kipato (Paundi) | Mshahara(Paundi) | Ziada (Paundi) | Mchezo | |
---|---|---|---|---|---|
1 | Floyd Mayweather | £66.11m | £66.11m | £0 | Boxing |
2 | Cristiano Ronaldo | £50.36m | £32.73m | £17.63m | Football |
3 | LeBron James | £45.52m | £12.15m | £33.37m | Basketball |
4 | Lionel Messi | £40.74m | £26.26m | £14.48m | Football |
5 | Kobe Bryant | £38.72m | £19.20m | £19.52m | Basketball |
6 | Tiger Woods | £38.53m | £3.9m | £34.63m | Golf |
7 | Roger Federer | £35.38m | £2.64m | £32.74m | Tennis |
8 | Phil Mickelson | £33.5m | £3.27m | £30.23m | Golf |
9 | Rafael Nadal | £28.02m | £9.13m | £18.89m | Tennis |
10 | Matt Ryan | £27.58m | £26.44m | £1.14m | American Football |
Post a Comment