Wajerumani, waliotumai wangefagia tuzo za Fifa na kubeba Ballon D'Or,
walieleza masikitiko yao Jumanne baada ya kipa wao aliyeshinda Kombe la
Dunia Manuel Neuer kuibuka wa tatu katika matokeo ya mchezaji bora wa
mwaka duniani wa mwaka 2014.
Mreno Cristiano Ronaldo alishinda tuzo hiyo kwa mara ya pili mtawalia Jumatatu na mara ya tatu kwa jumla.
Fowadi huyo wa Real Madrid alipata kura maradufu kumshinda mpinzani
wake wa jadi aliyeshinda tuzo hiyo mara nne Lionel Messi, ambaye
alimpiku pembamba kipa wa Bayern Munich Neuer aliyemaliza wa tatu.
Neuer, aliyewika sana katika Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka jana
na pia alisaidia Bayern kushinda ligi na kombe nyumbani, amefungwa mabao
manne pekee katika mechi 17 alizocheza ligini msimu huu.
“Nadhani si haki,” alisema nahodha na kocha wa zamani wa Ujerumani aliyeshinda Kombe la Dunia Franz Beckenbauer.
"Inaonekana kana kwamba katika kura hii ufanisi hauthaminiwi sana kama sura.”
"Makipa wamo katika pahala pagumu. Watu wanataka kuona mabao, si watu wanaozuia magoli yasifungwe.”
Ujerumani ilikuwa ikitarajia kufagia tuzo usiku huo baada ya kocha wa
timu ya taifa Joachim Loew kushinda tuzo ya kocha bora wa mwaka naye
kocha wa VfL Wolfsburg Ralf Kellermann akatawazwa kocha bora wa soka ya
wanawake.
Kiungo wa Wolfsburg Mjerumani Nadine Kessler alichaguliwa mchezaji bora wa mwaka wa kike.
“Nimetamaushwa kiasi kumhusu Manuel," Loew aliambia wanahabari. “Kwa
sababu katika Kombe la Dunia Manuel alionyesha mchezo tofauti sana wa
kulinda wavu na ni jambo ambalo halijawahi kufanyika awali.”
Neuer alitawazwa kipa wa mwaka 2014 baada ya ustadi wake Kombe la
Dunia, ambapo alitoka sana eneo la hatari na kufagia wapinzani tofauti
na makipa wengine wa awali.
Lakini hakuungwa mkono hata na wachezaji wenzake wa Bayern, straika
wa Poland Robert Lewandowski, kwa mfano akimpigia kura Mreno Ronaldo.
"Lilikuwa kosa kwangu kumpigia kura Ronaldo," Lewandowski aliambia
wanahabari baadaye. “Leo ningempigia kura Manuel lakini kura yangu
niliipiga Agosti. Ningepiga kura tofauti leo.”
Kwa Neuer, hata hivyo, ulikuwa usiku wa kufana hata bila yeye kushinda tuzo hiyo.
“Naondoka kutoka kwa jengo hili nikiwa na tabasamu kuu usoni.
Ilikuwa siku ya ushindi kwangu na ulikuwa ufanisi kuwa kwenye tatu
bora,” alisema. “2014 ulikuwa mwaka wa ufanisi mwingi na utasalia daima
akilini mwangu.”
Lakini wakati wajerumani wakitoa malalamiko yao hayo hizi ndizo kura zailizompitisha ronado kuwa mchezaji bora wa Dunia.
Chanzo: Supersport.com
Post a Comment