0
Klabu ya Fc Barcelona imetanga rasmi kumfuta kazi mkurugenzi wake wa masuala ya ufundi Andoni Zubizarreta. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu ya Barcelona hii leo kupitia kwa raisi wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu inasema kuwa Andoni ametimuliwa rasmi kuanzia hivi leo.

Raisi huyo alimshukuru Zubizarreta kwa utumishi wake uliotukuka kwa kipindi chote cha miaka minne alichoitumikia klabu hiyo lakini hakusita kumtupia lawama mkurugunzi huyo kwa kitendo cha klabu hiyo kujikuta ikiingia kwenye mgogoro wa kufungiwa na FIFA kutokufanya usajili wowote ule kwa kipindi cha miaka miwili kwa kosa la kumsajili mchezaji aliye chini ya miaka 18.

Ikumbukwe kuwa wiki iliyopita klabu ya Barca ilishindwa vibaya katika rufani yake iliyoikata kwenye mahakama ya usuruhishi wa masuala ya michezo (CaS) na hivyo kujikuta ikiwa inatakiwa kuitumikia adhabu ya kutosajili mchezaji yoyote mpaka mwezi wa Januari 2016.

Aidha raisi huyo hakusita kumshushia lawama mkurugenzi huyo na kumtaja kuwa ndiye aliyekuwa chanzo cha kuondoka kwa aliyekuwa meneja wa timu hiyi Pep Gardiola na sasa amekuja na balaa jingine la klabu kufungiwa kutokufanya usajili kwa miaka miwili kwa kosa aliloliita la kizembe la kumsajili mchezaji aliye chini ya umri wa miaka 18.


Post a Comment

 
Top