0

as_pogba2


Rais wa klabu ya Real Madrid Frorentino Perez anajiandaa kutoa ada inayotarajiwa kuvunja rekodi ya Dunia ya usajili ya kiasi cha paundi milioni 100 kwa klabu ya Juventus ya nchini Italia kwa lengo la kumnyakua kiungo raia wa Ufaransa anayekipiga kwa vibibi vizee hao Paul Pogba.

Taarifa zinadai kuwa raisi huyo yuko siriazi na jambo hilo na anachotaka kukifanya ni kurudia yale aliyoyafanya mnamo mwaka 2001 pale alipolipa kiasi kikubwa cha pesa kwa klabu hiyo kilichomng'oa kiungo bora wa muda wote Mfaransa Zinedine Zidane "Zizou" kutoka klabu ya Juve.

Ikumbukwe mapema wiki hii wakala wa kiungo huyo Mino Raiola alifunguka na kudai kuwa mustakabali mzima wa maisha ya soka aidha ndani au nje ya klabu ya Juve uko mikononi mwa Juventus wenyewe.

Post a Comment

 
Top