Radamel Falcao atachezea moja kati
ya timu bora duniani msimu ujao,hata kama haitakuwa Manchester United,
hayo ni maneno ya wakala wa Falcao, Jorge Mendes
Mchezaji huyu
mwenye umri wa miaka 28 alitokea Monaco na kujiunga na Man U kwa mkopo
mwezi Septemba lakini tangu wakati huo aliifungia Man U magoli matatu
pekee.
United wana muda mpaka mwezi June hapo wataamua kama wataendelea naye au la.
Nini maamuzi ya Falcao mwenyewe ?
Falcao mwenyewe ameshaamua kuwa hatarejea Monaco, yaani angependa kubaki United.
Hata hivyo, akiwa na United Falcao hakuwemo hata kwenye kikosi cha wachezaji 18 walipokutana na Southampton tarehe 11 mwezi huu.
Luis Van gaal amesema uamuzi wake uliegemea kwenye uchaguzi wa wachezaji ambao alihisi kuwa ndio bora zaidi kwa mchezo huo.
Post a Comment