Mchezaji wa kiungo cha kati katika
kilabu ya Chelsea Cesc Fabregas anaamini kwamba Lionel Messi hataondoka
katika kilabu ya Barcelona.
Chelsea imehusishwa na mchezaji huyo kufuatia madai kwamba amekuwa akizozana na Kocha Luis Enrique.
Lakini
Fabregas ambaye ni rafiki wa karibu wa mchezaji huyo wa Argentina
hafurahii madai ya vyombo vya habari kwamba anajaribu kumshawishi Messi
kujiunga na The Blues.
''Messi anafurahia kuwa Barcelona na Barcelona inafurahia kuwa naye'',alisema mchezaji huyo wa Uhispania.
''Nimeshangazwa
kwamba mimi najaribu kumvuta Messi katika kilabu ya Chelsea kwa niaba
ya Chelsea,nitawezaje kuzungumza kuhusu kandarasi na mimi ni mchezaji
tu''.aliuliza.
Post a Comment