Vigogo Manchester United watajaribu kuzima ushindani mkubwa wa nafasi
ya tatu kwenye daftari ya ligi ya Premier ya Uingereza kutoka
Southampton watakapowaalika kasri yao ya Old Trafford kwa kivumbi
kikubwa Jumapili.
United wamefuatanisha mechi 10 bila kuonja kichapo tangu kukomeshwa
1-0 na mabingwa Manchester City Novemba 2 mwaka uliopita lakini wamezoa
alama sita pekee kutoka 12 baada ya kutoka sare mara tatu kwenye mechi
nne za mwisho.
Mtindo huo umekaba vijana wa Louis van Gaal kufaidika na kuteleza
kwa viongozi Chelsea wanaowafuata na alama 12 na kuwapatia Southampton
nafasi ya kuwakaribia kwa tofauti ya pointi moja pekee.
Baada ya kuchapwa mara nne mtawalia kati ya Novemba mwishoni na
mwanzo wa Desemba ikiwemo kulazwa 2-1 kwenye mkondo wa kwanza wa mechi
hii, kikosi cha Ronald Koeman kimeshinda mechi tatu na kutoka sare dhidi
ya Chelsea katika ngoma zao nne za mwisho.
United walibahatika kushinda St Mary’s mwesi jana wakati magoli
mawili ya straika Robin van Persie yalipowakilisha makombora matatu
pekee langoni la Southampton katika dakika 90.
United wameshamiri pakubwa mwezi mmoja uliopita na jinamizi la
majeraha limewaondokea huku Ashley Young akiwa kiungo pekee ambacho
hatakuwa tayari kucheza mechi hii huku kikosi hicho kikipata kiinua
mgongo kwa kusaini kwake kipa maarufu Victor Valdes aliyetamba na
Barcelona.
“Nina mchezaji mmoja pekee aliyeumia (Young) lakini sina kikosi
kamili cha asilimia 100 ambacho kina usawa wa mechi,” Van Gaal
alitahadharisha.
Chanzo: Supersports.com
Post a Comment