Kocha wa timu ya taifa ya soka
Tanzania, Mdachi Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 26
kitakachoivaa Rwanda katika mechi ya kirafiki itakayochezwa Mwanza hapo January
22.
Mechi hiyo itakuwa ni sehemu ya maandalizi kwa timu zote kwa
ajili ya kujiandaa na michuano ya kufuzu kucheza fainali za Afrika
(CHAN) kwa wachezaji wa ndani (un-professionals) itakayoanza mwezi wa 5
mwaka huu ambapo Rwanda itakuwa mwenyeji fainali hizo zitakazofanyika mwakani.
Walioteuliwa ni wachezaji waliochini ya miaka 22 wakiwa ni sehemu ya matayarisho ya kucheza timu ya taifa miaka ijayo.
Wachezaji
hao na timu zao katika mabano ni makipa Aishi Manula (Azam), Benedict
Tinoco (Kagera Sugar), Peter Manyika (Simba).
Wakati mabeki ni Miraji
Adam, Andrew Vincent (Mtibwa Sugar), Gadiel Mbaga (Azam), Emmanuel
Semwanda (African Lyon) Joram Mgeveke ( Mwadui), Salim Mbonde (Mtibwa
Sugar) na Edward Charles (Young Africans).
Viungo ni Salum Telela (
Yanga) , Adam Salamba (Bulyankulu FC) wakati Hassan Banda, Mohammed
Hussein, Said Makapu na Said Ndemla wakiwa ni wachezaji wa Simba Sports
Club.
Viungo wengine ni Hussein Malombe (Geita Gold SC), Shiza
Ramadhani (Mtibwa Sugar), Omar Nyenje (Ndanda FC), Hassan Dilunga
(Yanga) na Alfredy Masumbakenda ( Bulyankulu SC).
Washambuliaji ni
Aboubakar Mohammed (White Bird), Kelvin Friday (Azam FC), Simon Msuva
(Yanga), Atupele Mwaisemba na Rashid Mandawa (Kagera Sugar).
Timu
hiyo itakuwa na kambi mbili, moja itakuwa Dar es Salaam na baadhi ya
wachezaji watafanya mazoezi Mwanza. Kambi hizo zitaanza Jumapili.
Post a Comment