Nahodha wa Liverpool
Steven Gerrard amesema angelikubali kusalia katika klabu hiyo iwapo
angekabidhiwa mkataba mpya kabla ya mwanzo wa msimu.
Nyota huyo wa miaka 34 alitangaza wiki iliyopita kwamba atagura klabu
hiyo na kuhamia Ligi Kuu ya Soka la Marekani almaarufu MLS baada ya
kukaa maisha yake yote ya uchezaji katika klabu hiyo ya Merseyside.
Gerrard alisema wikendi kwamba alifikia uamuzi wa kuondoka pale
meneja Brendan Rodgers alipomwambia hangekuwa akicheza kila mechi.
Hakulaumu klabu hiyo kwa uamuzi wake wa kuondoka lakini alisema
alikuwa tayari kujitolea kukaa zaidi Liverpool hasa baada yao kumaliza
nambari mbili ligini msimu uliopita.
“Iwapo mkataba ungebwagwa mezani kabla ya msimu kuanzia ningeutia
saini,” Gerrard alinukuliwa akisema na Liverpool Echo Jumanne.
"Nilikuwa ndio tu nimestaafu soka ya kimataifa Uingereza ili
kuelekeza juhudi zangu zote Liverpool. Sikutaka kupimiwa mechi katika
klabu.
“Rekodi yangu ya majeraha imekuwa shwari kwa miaka miwili na nusu na
nilikuwa na msimu wa kufana, kwa maoni yangu binafsi, msimu uliopita.
“Hayo yote sasa yamepita. Kipindi hicho kati ya majira ya joto na Novemba kilinipa muda wa kutafakari.
“Simlaumu yeyote na sina hasira wala chuki. Kuna watu wengine kwenye kikosi na klabu ina mengine ya kujishughulisha nayo.
“Simlaumu meneja au mtu mwingine yoyote katika klabu.”
Gerrard, aliyefunga mabao mawili Jumatatu na kusaidia Liverpool kulaza
AFC Wimbledon 2-1 na kufika raundi ya nne ya Kombe la FA, anakaribia
kutia saini mkataba wa miezi 18 na klabu ya Los Angeles Galaxy, kwa
mujibu wa ripoti kwenye vyombo vya habari.
Chanzo
Post a Comment