Makamu wa Rais wa shirikisho la soka
duniani, Mwanamfalme Ali Bin Al Hussein wa Jordan, amesema kuwa
atamenyana na Sepp Blatter kuwania urais wa shirikisho hilo.
Ali Bin Al Hussein amesama atagombea urais wa shirikisho hilo katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Mei.
Sepp Blatter anawania urais wa shirikisho hilo kwa muhula wa tano.
Kwa
upande wake, Ali Bin Hussein, huenda akapokea uungwaji mkono wa
mashirikisho ya soka Ulaya ingawa haijabainika ikiwa ataungwa mkono na
shirikisho lenye nguvu sana la soka ya Bara Asia.
Mwanamfalme
huyo, amesema ni wakati sasa wa kubadilisha mambo katika shirikisho hilo
hasa kutokana na kashfa nyingi ambazo zimekumba soka duniani.
Alikuwa
akigusia madai ya rushwa ambayo amehusishwa nayo, bwana Blatter na
kutikisa uongozi wake wa shirikisho hilo kwa miaka 17 iliyopita.
Mwanadiplomasia wa Ufaransa Jerome Champagne, pia anajiandaa kuwania uongozi huo dhidi ya wawili hao.
Post a Comment