Mgombeaji wa kiti cha urais wa Fifa, mwana wa mfalme Ali bin Al
Hussein ameeleza imani ya kumgatua Sepp Blatter mamlakani mwezi Mei huku
akikemea uendeshaji wa shirikisho hilo la kandanda duniani kwa ‘siri’.
Maafisa wakuu wa bara lake Asia wamepuuzilia ugombeaji wa mwana huo
wa ufalme wa Jordan lakini Ali alibashiri manifesto yake ya kusafisha
sifa mbaya ya Fifa machoni mwa dunia utashawishi washirika kumpigia kura
kwenye uchaguzi wa Mei 29.
“Tarakimu hazinitatizi kwa sasa. Tuna miezi kadhaa kabla ya
uchaguzi mwenyewe lakini nina imani kamili kuna watu wa msimamo mwema
ambao watapigia utawala wa siku za usoni wa kandanda,” alisema.
Ingawa rais wa shirikisho la kandanda la Asia, AFC, president Shaikh
Salman bin Ebrahim Al Khalifa ametangaza hatua yao ya kuunga mkono
Blatter kwa dhati hatobadilika, Ali aliendelea na kilio chake cha uwazi
zaidi ndani ya Fifa.
“Fifa kama shirikisho lina uzoefu wa siri. Lakini kandanda ndio
mchezo maarufu zaidi duniani na tunastahili kuwa na imani na kufurahia
uwazi na kila mtu. Sioni sababu ya kuendeleza kisirisiri.”
Post a Comment