Jumla ya mashabiki 40,000 walihudhuria kwenye dimba la nyumbani la klabu ya Atletico Madrid la Vicente Carderon kumlaki kwa mara ya pili shujaa wao wa miaka mingi aliyekua ametimukia ughaibuni Muhispania
Fernando Torres.
Jambo hili linaweza likawa la ajabu sana miongoni mwa mashabiki wa klabu ya Chelsea lakini walichokifanya mashabiki wa klabu ya Atletiko ni kuonesha kiasi cha upendo walichonacho kwa Muhispania mwenzao ambaye wanamuona kama amegeuzwa mbuzi wa kafara na klabu ya Chelsea.
Torres, alijitengenezea jina kubwa sana alipokua akiitumikia klabu hiyo pale ambapo alipofanikiwa kuifungia jumla ya magoli 82 kwenye michezo takribani 214.
Hii ni mara ya kwanza kwa mshambuliaji huyo kurejea Vicente Calderon tangu mwaka 2007 na huenda akapata faraja kubwa kutokana na mapokezi ya kishujaa aliyoyapokea kutoka kwa mashabiki hao.
Post a Comment