Mwamuzi mstaafu Howard Webb hatimaye amewapasha watu wliokuwa wakimtuhumu kuwa yeye ni mnazi wa Mashetani wekundu wa Manchester United.
Ikumbukwe kuwa kiungo wa zamani wa klabu ya Liverpool Rayan Babbel aliwahi kutozwa faini ya paundi 10000 kwa kosa la kuchapisha picha kwenye mtandao wa twetter zikimuonesha Webb akiwa amevalia jezi ya United mara baada ya kufungwa kwenye mchezo wa kombe la FA mchezo ambao ulichezeshwa na Webb.
Webb aliyejiuzulu kuchezesha mpira wa miguu wiki iliyopita na kupewa majukumu mapya ya kuwa mkurugenzi wa ufundi wa chama cha waamuzi amejibu mapigo kwa kusema kuwa kamwe yeye hakuwa shabiki wa Manchester United, na kamwe hakuwa akiipendelea klabu hiyo kwenye maamuzi yake.
"Ni vitu vyenye aina fulani ya ukweli ndani yake, lakini hakikuwa kitu kinachoniathili wala kuwa ndani ya akili yangu, haikuwa sumu bali yalikua ni manemo ambayo siku zote huwa ni chakula cha ulimi"
"kilichokua kikisalia ndani akili yngu ni pale nilipokua nikifanya makosa na haswa nilipogundua kuwa kosa hilo limebadili matokeo ya mchezo husika, nitakua sio mkweli kama nisiposema kuwa yalikua yakinisumbua akilini mwangu, haswa gaazeti lililo orothesha michezo mitano ambayo nilifanya makosa lakini huwa napata faraja ninapogundua kuwa nina orodha ndefu ya michezo takribani 500 ambayo mimi nimeisimamia katika ngazi mbalimbali, faraja pia huwa inaongezeka pale ninapogundua kuwa wako wachezaji wa mpira wa miguu waliofanya makosa makubwa lakini bado wanabakia kuwa na sifa na heshima zao katika maisha yao yote hata mara baada ya kuachana na soka"
Webb
alikua akichukuliwa na FIFA na Premier League kama mmoja kati ya waamuzi bora kuwahi kutokea Duniani kwani katika maisha yake ya uamuzi amekwisha chezesha fainali mbili za kombe la dunia na moja kati ya hizo akichezesha mchezo wa fainali.
Post a Comment