Diego
Simeone amepewa adhabu ya mwana ukome ya kutokukaa katika benchi la ufundi kwa michezo minane baada kutolewa nje kwa kosa la kumpiga kibao cha kisogoni mwamuzi wa mezani (fourth official) kwenye mchezo ambao ulishuhudia timu yake ta Atletico Madrid wakitwaa ubingwa wa Super Cup dhidi ya mahasimu wake wakubwa Real Madrid hapo siku ya Jumaatano.
Taarifa zilizotolewa na mabosi wa chama cha soka cha huko nchini Uhispania zimesema kuwa Simeone anafungiwa michezo minne kwa kosa la kumpiga kofi mwamuzi huyo mara baada ya kuisha kwa kipindi cha kwanza Michezo miwili kwa kosa la kupinga maamuzi na mchezo mmoja kwa kosa la kuwapa maelekezo wachezaji wake akiwa jukwaani akiitumikia adhabu yake na mchezo mmoja kwa kosa la kuzomea maamuzi.
Adhabu hiyo ya Simeone inaambatana na faini ya Euro 4,805 (Paundi 3,800), Wakati klabu yake ya Atletico Madrid nayo imepigwa faini ya Euro 2,800 (Paundi 2,230).
Simeone sasa anatakribani siku kumi kukata rufani ya kupinga adhabu hiyo ambayo itahusisha michezo yote ambayo chama cha soka cha nchini Spain itakua inahusika kwa namna moja au nyingine.
Post a Comment