Newcastle imeitaja thamani halisi ya kiungo wake raia wa Ivory Coast Cheick Tiote kuwa ni paundi milioni 14 na sio 4 kama ambavyo klabu ya Lokomotiv Moscow ya kule nchini Urusi iliweka ofa mezani.
Warusi hao wanamtaka Tiote ambaye wanamuona kuwa ni mbadala sahihi wa Lassana Diarra anayewindwa kwa udi na uvumba na Queens Park Rangers.
Bosi wa The Gunners Arsene Wenger kwa sasa ameingia sokoni kwa minajiri ya kumsaka kiungo mkabaji ili kuongeza ufanisi kwenye timu yake na Tiote ambaye anatajwa kuwa ni mmoja kati ya viungo hodari kwa kazi hiyo anaonekana kuwa kwenye rada za Mfaransa huyo.
Kwa siku za hivi karibuni klabu ya Arsenal imekua ikitajwa kuhusika na dili la kutaka kuwanyakua viungo wa Magaraktiko wa Real Madrid Sami Khedira na mwingine kutoka klabu ya Sporting Lisbon William Carvalho kwenye majira haya ya kiangazi lakini sasa inaonekana wamegundua kuwa Tiote atakua na gharama nafuu zaidi ukilinganisha na wachezaji hao wawili na hivyo kuwa mbadala sahihi kabisa.
Post a Comment