0
as_ancelotti
Klabu ya Real Madrid ya huko nchini Hispania iko katika hatua za mwishomwisho kuitafuta klabua ambayo itakua tayari kumnunua kiungo mjerumani anayekipiga katika timu hiyo Sami Khedira siku chache zijazo ndani ya mwezi huu.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani amegoma kuzungumzia kuhusiana na suala la yeye kusaini mkataba Mpya na Les Blancos licha ya ukweli kwamba mkataba wake mpya huo unatarajia kuisha majira ya kiangazi yajayo.

Arsenal na Chelsea ni moja kati ya timu ambazo tayari zimeonesha nia ya kutaka kuzipata huduma za kiungo huyo asiyekua na mambo mengi awapo uwanjani.
 
Tayari vilabu hivyo kwa nyakati tofauti vilikwisha tuma ofa ya paundi milioni 25 kwa klabu ya Madrid  kwaajili ya Khedira, lakini Madrid walizipiga chini ofa hizo kwakile wanachokidai kuwa hazifanani na thamani halisi ya mchezaji mwenyewe.

Khedira kuanzia January mosi mwakani atakua yuko huru kufanya mkataba wa awali na klabu yoyote ile nje ya Uhispania hali inayowafanya Real kuhaha kuitafuta klabu itakayokuwa tayari ilimradi waambulie chochote kutoka kwa mchezaji huyo.

Tayari klabu ya Real Madrid inamtazama Asier Illarramendi kama ndiye mrithi mpya wa nafasi ya Sami Khedira ndani ya klabu hiyo.

Post a Comment

 
Top