0
Skippers: Wayne Rooney and Steven Gerrard lead the teams out at the Sun Life Stadium in Miami Gardens


Pepe Reina anatarajiwa kukamilisha uhamisho unaokadiliwa kufikia paundi milioni 2 kujiunga na mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich, kwa mujibu wa mtendaji mkuu wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge.

“Ndio tumekwisha fanya makubaliano na dili liko tayari ," alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya ujerumani akiwa mjini Portland nchini Marekani kwenye ziara ya maandalizi ya msimu mpya na klabu hiyo.

"Reina ni golikipa wetu mpya kwa sasa. Ni mzoefu na anafurahia kuja Munich, licha ya kuwa Manuel Neuer ndiye golikipa wetu namba moja.


Reina, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 31 ameitumikia timu ya taifa ya Hispania jumla ya michezo 33, siku za karibuni alikua pia akihusishwa na klabu ya AC Milan na Napoli ambako alikuweko msimu uliopita akicheza kwa mkopo akitokea Liverpool.

Meneja wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers amemkabidhi milingoti Simon Mignolet hali inayomfanya Reina kuwa kama mchezaji wa ziada ndani ya klabu hiyo ya Merseyside.

Anakwenda kuungana na meneja wa Bayern, Pep Guardiola ambaye alicheza nae Barcelona miaka kadha iliyopita wakati wawili hao walipokua wakicheza soka nchini Spain.

Reina aliyezaliwa na kukulia Madrid alijiunga na Barcelona,ambako akiwa kijana mdogo alicheza takriban michezo 30 na kikosi cha kwanza lakini alipotimiza umri wa mika 20 alianza kuonekana hatoshi ndani ya Barca na kuanza kutumika kama ziada pale ambapo timu hiyo iliamua kumuajiri golikipa Mjerumani  Robert Enke mwaka 2002.

Reina alijiunga na Villarreal, ambako alicheza jumla ya michezo 136 ndani ya misimu mitatu na kuuthibitishia ulimwengu wa kabumbu kama mmoja kati ya magolikipa hodari sio Spain tu bali duniani kwa ujumla ambapo mwaka 2005 alicheza mchezo wake wa mwanzo wa kimataifa; na uhamisho wa pesa nyingi kwenda Liverpool ukafuata lakini mara baada ya usajili wa Mignolet ndani ya Merseyside majira ya kiangazi alikataa kuongeza mkataba na Liverpool na kuamua kwenda kucheza kwa mkopo kwenye klabu ya Napoli  inayoshiriki ligi ya Serie A.

Wakati fulani Reina alihusishwa sana na kurejea Barca lakini usajili wa Marc-Andre ter Stegen na Claudio Bravo ulikatisha tumaini la Reina kurejea Barcelona.

Post a Comment

 
Top