Klabu za Liverpool na Manchester United zinaweza zikajikuta zikiingia vitani tena siku chache zijazo. Safari hii itakua ni vita ya nje ya uwanja wote kwa pamoja wakiwa wanawania saini ya mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Borussia Dortmund Marco Reus.
Uwezekano wa kutokea kwa vita hiyo unakuja kutokana na kuvuja kwa mkataba baina ya mchezaji Marco Reus na BvB ambapo kipengele kinachoruhusu kuvunjwa kwa mkataba kimeanikwa hadharani.
Taarifa za uhakika zinasema kuwa kipengere hicho kinamuweka huru Reus kutimkia timu ambayo itakua iko tayari kutoa kitita cha paundi milioni 19.8. Halikadhalika mchezaji mwenyewe anaweza kulazimisha uhamisho wake na kwakufanya hivyo timu itakayokua inamuhitaji italazimikakulipa kiasi cha paundi milioni 30.
Hali hiyo inafungua milango kwa mahasimu hao wawili wa kuanza kuifukuzia saini ya mshambuliaji huyo wa Kijerumani ambaye pia amekua akiwindwa kwa ukaribu sana na vilabu vya Bayern Munich na Real madrid ili kuimarisha vikosi vyao ambapo rasmi kipengele hicho kitaanza kufanya kazi majira ya kiangazi yajayo.
Bosi mpya wa klabu ya Manchester Luis van Gaal yuko kwenye mawindo ya mwishomwisho ya kukiimarisha kikosi chake ukiwa ni msimu wake wa mwanzo kuongoza klabu ya ligi kuu nhini Uingereza ambapo siku za hivi karibuni mara baada ya ziara yake ya kutoka huko nchini marekani amehusishwa na kuwataka wachezaji kadhaa Reus akiwa mmoja wapo.
Reus aliyejiunga na Dortmund mnamo mwaka 2012 akitokea klabu kikine cha Kijerumani Borussia Monchengladbach baada ya klabu yake kiyo ya nyumbani kumuachia bure kama mchezaji aliye chini ya miaka 17 amefunga takribani magoli 21 katika michezo 39 aliyoichezea Dortmund kwa msimu uliopita na alikua miongoni mwa wahezaji 23 wa walioteuliwa kuunda kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani lakini alishindwa kusafiri na wenzake mara baada ya kupata majeruhi akiwa katika michezo ya maandalizi.
Lakini wadadisi wa mambo wanasema timu ambayo inaonekana kana kwamba ina nafasi kubwa ya kumtwaa mchezaji huyu ni bayern Munich kwakuwa reusi alinukuliwa na moja kati ya magaazeti ya huko ujerumani akiifagilia timu hii kuendelea kulitawala soka la barani Ulaya na pia ligi ya ujerumani kwa mara nyingune tena.
"Nionavyo mimi bado Bayern wataendelea kutawala kwakuwa wanaongeza ubora wa kikosi chao na sio kupunguza ubora wao, wanasajili watu ambao watakwenda kuisaidia timu kuwa na makali zaidi"
"Ukitazama msimu uliopita tumemaliza tukiwa na alama 19 nyuma ya Bavarians na ili kuwafikia msimu ujao tunatakiwa kuwa makini na kuhakikisha kuwa hatupotezi alama yoyote kwenye michezo yetu."
Post a Comment