Loic Remy amekamilisha uhamisho wa paundi milioni 8 na rasmi sasa anatua darajani kama mbadala wa Fernando Torres aliyetimukia klabu ya AC Milan ya huko nchini Italy kwa mkopo.
Mara tu baada ya kuondoka Torres, Mourinho haraka alimtafuta mbadala wake ambaye hakuona mtu mwingine isipokuwa Remy ambaye alikua na kipengere kwenye mkataba wake kinachomruhusu yeye kuondoka ndani ya QPR iwapo tu itatokea klabu itakayolipa kitita cha paundi milioni 10.5.
Taarifa zinasema kuwa Remy sasa anatarajiwa kuweka kibindoni kiasi cha paundi elfu 80,000 kwa wiki.
Harry Redknapp amemuacha Remy kwenye kikosi kilichoivaa Sunderland mchana wa leo na alipoulizwa na waandishi wa habari kwa kifupi sana alijibu kuwa Remy anaondoka.
Post a Comment