MATUSI YA MASHABIKI WA ARSENAL NI UJINGA MTUPU-NASRI. 11:25 Unknown 0 FOOTBALL A+ A- Print Email Katika hali inayoonesha kama haofii na changamoto za nje ya uwanja kuelekea kwenye mchezo wa Ngao ya hisani baina ya timu yake ya Manchester City na timu yake ya zamani ya Arsena kiungo Mfaransa Samir Nasri amesema kuwa kamwe haathiliki na kelele na matusi ya mashabiki hao na kuuita kuwa ni ujinga mtupu. Kiungo huyo aliyihama klabu hiyo mnamo mwaka 2011 amekuwa ni mtu anayezomewa sana na mashabiki wa klabu ya Arsenal kila mara ambapo timu hizi zinapokutana. "Matusi kamwe hayaniathili mimi ndani ya uwanja, ninaona kama ni ujinga mtupu kwangu mimi, Mimi sio shabiki wa Arsenal, Sitoki London bali mimi ni mchezaji ambaye nanaangalia mambo mengi kabla sijafanya maamuzi ya kusaini mkataba na klabu yoyote ile." "wakati Manchester City walipokuja na kutaka kunisajili niliangalia baadhi ya mambo binafsi na kuona kuwa hapa ni mahala na chaguo sahihi kabisa kwangu kuja hapa, na sasa unaweza kuona tayari nimekwisha shinda mataji kadhaa, nina kila kitu na pia maisha yangu ni mazuri pia. Wachezaji kadha wa arsenal wameondoka kwenye klabu hiyo kwa nyakati tofauti wakiwemo Bacary Sagna,Emmanuel Adebayor, Kolo Toure,na Clich. Alipoulizwa kama klabu yake hiyo ya zamani inaweza kuwa mabingwa msimu huu bila kusita alijibu kuwa hadhani kama Arsenal wanaweza kuwa mabingwa kwani wana mapungufu makubwa kwenye ulinzi na pia sehemu ya kiungo cha ukabaji.
Post a Comment