Meneja wa vibibi vizee vya kutoka mji wa Turin (Juventus) Massimiliano Allegri amesema anafikiria kumbadilishia majukumu ya kiuchezaji kiungo Mfaransa Paul Pogba kwenye msimu mpya wa ligi kuu ya kule nchini Italy na michuano ya mabingwa barani Ulaya (Uefa champions League).
Allegri anaamini kuwa kutokana na majukumu mapya hayo anayotarajia kumkabidhi kiungo huyo anatarajia kupata magoli mengi zaidi kutoka kwa kiungo huyo mwenye nguvu na misuli iliyojengeka.
"Nitamtumia kama mshambuliaji zaidi tofauti na alivyokua anatumika awali kama kiungo mkabaji, Ni mmoja kati ya viungo bora chipukizi kwa sasa Duniani aliyejawa na ufundi mwingi na nguvu nyingi."
Meneja huyo mpya wa Juve aliendelea kusisitiza kuwa viungo wake wawili Arturo Vidal na Paul Pogba wana furaha kubwa kuwa sehemu ya juventus na yeye kama mwalimu anafurahi sana kuwaongoza wachezaji wa kalba yao wenye uwezo wa hali ya juu.
Siku za hivi karibuni wachezaji hao wawili wamekua wakihusishwa na vilabu mbalimbali barani Ulaya kutokana na kiwango cha kiuchezaji cha hali ya juu kilichooneshwa na wanandinga haopindi wawapo dimbani.
Vilabu vya chelsea,Manchester United, Real Madrid, Arsenal, PSG na Barcelona ni miongoni mwa vilabu kadhaa vilivyoonesha nia ya kutaka kuwasainisha wanandinga hao wawili.
Post a Comment