Kiungo wa Juventus Mauricio Isla ameichelewesha safari yake katika jiji la London kwaajili ya mazungumzo na klabu ya Queens Park Rangers kama ilivyokubaliwa.
Kiungo huyo mwenye asili ya Chile ilikua atue jijini london kwa minajili ya kufanyiwa vipimo vya afya na kusaini mkataba wa mkopo kabla ya kusaini mkataba wa moja kwa moja hapo baadae.
Ikumbukwe pia QPR ilikua kwenye mazungumzo mzito na kibibi kizee cha Turin (Juventus) ili pia waweze kumnasa mshambuliaji wa kiitaliano Sebastian Giovinco ili nae aweze kujiunga na timu hiyo kwa mkopo lakini mshambuliaji huyo ameamua kubakia katika jiji la Turin.
Post a Comment