0
as_vidal

Kiungo raia wa Chile anayekipiga kwenye klabu ya kibibi kizee cha Turin (Juventus) Arturo Vidal amekubali mkataba wa awali wa mashetani wekundu kutoka jiji la Manchester. 

Gaazeti la kila siku la mjini Turin La Stampa limeandika kwamba Vidal amekwisha washiwa taa ya kijani na mashetani wekundu hao ambao wamemuahidi mkataba mnono utakao ambatana na mkataba wa miaka mitano ambao utamfanya Vidal kujinyakulia kitita cha paundi 182,000 kila wiki.

Mabingwa hao wa Italia wanahitaji majibu kutoka kwa Vidal binafsi kama anasalia ndani ya Juve au anataka kutimuka ndani ya vibibi vizee hao.

Klabu ya Manchester United imepanga kuvunja rekodi yake ya usajili iliyopo klabuni hapo ili kuinasa saini ya Mchile huyo mwenye mambo machache na yenye uhakika awapo uwanjani. 

Taarifa zinasema kwamba mashetani wekundu hao wako tayali kuwapa Juve kitita kinachakadiliwa kufikia paundi milioni 47 kwaajili ya kupata huduma za Vidal.

Post a Comment

 
Top