Daley Blind anatarajia kujiunga na klabu ya Manchester United kutoka klabu ya Ajax kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 13.8.
Vilabu hivi viwili vimeshafanya makubaliano ya kimsingi hapo jana juu ya suala la uhamisho wa mchezaji huyu na kinachosubiriwa sasa ni makubaliano binafsi baina ya Manchester United na mchezaji Delay Blind.
Blind
hajajumuishwa kwenye kikosi cha klabu ya Ajax kinachotarajiwa kuvaana na klabu ya Groningen kwenye mchezo wa ligi kuu ya nchini Uholanzi hapo kesho.
Hii inatokana na klabu ya Ajax kumruhusu mchezaji huyu kwenda kufanya makubaliano binafsi na klabu ya Manchester juu ya uhamisho wake.
Ikiwa mambo yatakwenda sawa basi Blind anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya hapo kesho kwenye mji wa Manchester kabla ya dili la uhamisho wake kukamilishwa rasmi.
Ujio wa Blind unakwenda kutimiza idadi ya wageni watano ndani ya United ambao ukiwahusisha pia wachezaji Angel di Maria, Marcos Rojo, Ander Herrera na Luke Shaw kwenye majira haya ya kiangazi ambapo uhamisho huu unakwenda kukamilisha kiasi cha paundi milioni 150 kutumika na Manchester United kwenye majira haya ya kiangazi.
Post a Comment