Luis Suarez alionekana kutokwa na jasho jingi leo hii pale alipokua kwenye mahakama ya rufani ya masuala ya michezo CAS pale nchini Switzerland. Suarez aliyeambatana na wanasheria wake mahakamani hapo alikwenda mahususi kwa kusikiliza rufani yake ya kufungiwa michezo miezi minne mara baada ya kumng'ata Muitaliano Georgio Chiellini.
Suarez akiwa na wawakilishi wake walikuwepo mahakamani hapo wakijaribu kushinikiza kupunguzwa au kufutwa kwa adhabu hiyo kali inayomkabili mshambuliaji huyo mpya wa Barcelona na tinu ya taifa ya Uruguay.
Kesi hiyo iliyosikilizwa kwa takribani masaa sita ilionekana kumuendea vigumu mshambuliaji huyo.CAS imesema kuwa mara baada ya shauri hilo kusikilizwa wanajaribu kukaa na kufanya mapitio ya vipengele mbalimbali na wanatarajia kutoa majibu ya rufani hiyo kabla ya wiki hii kumalizika.
Lakini mwanasheria wa chama cha soka cha Uruguay amesema kuwa yeye na mtetezi wake wanatarajia kuwa CAS itatangaza maamuzi ya rufani hiyo ndani ya siku kumi ili mteja wake aanze kutekeleza majukumu yake.
Post a Comment