Anawindwa: Javier Hernandez (kushoto) yupo katika rada za Southampton ambao wamepanga kutumia paundi milioni 70 majira haya ya kiangazi.
Southampton wanapanga kutumia paundi milioni 70 siku chache zijazo ili kusajili wachezaji wataoziba nafasi za nyota wao walioondoka.
Saints wanatarajiwa kuwasajili baadhi ya wachezaji watakaoachwa na Manchester United wakati huu wanaoimarisha kikosi chao.
Klabu hiyo inamhitaji mshambuliaji wa Mexico, Javier Hernandez na Wilfried Zaha au Ashley Young kutegemeana na winga gani Louis Van Gaal atamuacha.
Bosi mpya wa Saints, Ronald Koeman pia anaziwinda saini za waholanzi wawili, Ron Vlaar wa Aston Villa na Virgil van Dijk wa Celtic, wakati huo huo kipa wa Celtic Fraser Forster naye yupo katika rada zake.
Tatizo la Southampton ni kwamba klabu nyingine zitawasumbua kwenye dau la uhamisho kwasababu zinajua timu hiyo imepata paundi milioni 100 baada ya kuuza wachezaji watano wa kikosi cha kwanza.
Post a Comment