0

as_lampard

Meneja wa klabu ya Chelsea  Jose Mourinho amesema hadhani kama Cesc Fabregas ndiye mbadala wa Frank Lampard.Cesc aliyewasili darajani mwanzoni mwa majira haya ya joto akitokea klabu ya Barcelona ya kule nchini Hispania amekua akizungumzwa kama mrithi wa Lampard pale darajani.

Mashabiki wengi wa mpira wa miguu hasa wale wa timu ya Chelsea wanajaribu kuwafananisha watu hao wawili na wamekua wakihusisha kuondoka kwa Lampard kama ni kuzikimbia changamoto za kijana huyo ambaye sio mgeni kwenye ligi kuu ya Uingereza'


Mourinho amesema  "Fabregas ni aina ya mchezaji ambaye klabu ya Chelsea inamuhitaji kwa sasa ili kuweza kufikia malengo yetu ya kujikusanyia vikombe mbali mbali lakini sidhani kama yeye atakwenda kuwa mrithi wa Frank klabuni kwetu"

"Lampard ni aina ya kipekee ya kiungo ambaye ili kufikia daraja lake inakulazimu ufanye mambo mengi na makubwa kwenye klabu yako kitu ambacho Cesc bado hajakifikia"

Siku za hivi karibuni kumeibuka hisia tofauti mara baada ya Lampard kusajiliwa kwa mkopo wa miezi sita kutoka klabu ya New York City ambapo mashabiki wengi wa klabu ya chelsea wanamchukulia Lampard kama muhaini kwa kuwa iko siku atakuja kuvaa jezi ya Man City kwenye mchezo dhidi ta Chelsea inayomchukulia yeye kama moja ya alama yake.


Post a Comment

 
Top