0

WAKATI timu nyingi zikiwemo Real Madrid, PSG, Barcelona, Bayern Munich, Juventus na FC Zenit, zimejihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, mambo yamekuwa tofauti kwa mashetani wekundu wa jiji la Manchester klabu ya Manchester United.

Klabu hiyo ya Old Trafford ilihitaji kushinda kwenye uwanja wake wa nyumbani dhidi ya PSV Eindhoven ili kuwa na uhakika wa kufuzu kwaajili ya hatua ya 16 bora, lakini ikaambulia sare ya 0-0.

United imebaki nafasi ya pili ikiwa na alama 8 na sasa itakuwa na kibarua kigumu cha kuifunga Wolfsburg inayoongoza kundi B hapo Disemba 8.

Klabu nyingine ya Uingereza, Manchester City nayo imejichelewesha kutinga katika hatua hiyo ya 16 bora baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa kibibi kizee cha mji wa Turin nchini Italia  Juventus kwenye mchezo wa kundi D.

Post a Comment

 
Top