0

Tetesi kuwa aliyewahi kuwa kocha wa timu za Napoli na Inter Milan Walter Mazzarri kuwa muda mfupi ujao atakua anafanya kazi nchini Uingereza zimezidi kushika kasi na kwa kiasi fulani kuendelea kuthibitika mara baada ya kuvuja kwa taarifa kuwa anaishi na familia yake jijini Manchester.

Mazzarri aliiongoza  Napoli mpaka nafasi ya pili katika mbio za ligi kuu nchini Italia nyuma ya kibibi kizee cha Turin Juventus mnamo mwaka 2013 kabla ya kuondoka kuelekea kwenye klabu ya Inter ambako aliambulia kutimuliwa na Nerazzurri hao mnamo mwezi wa November 2014.

Mazzarri, ambaye ataendelea kulipwa na klabu ya Inter Milan mpaka mwaka 2016 mnamo mwezi Juni amehamia Uingereza mnamo mwezi Juni mwaka huu kwa mujibu wa mtandao wa calciomercato.

Taarifa zinadai kuwa Mazzarri amehamia kwenye jiji la Manchester kwa malengo ya kuzifuata klabu mbili kubwa za jiji hilo lakini pia kwa matilaba ya kukiboresha kingereza chake. 

Mazzarri anatajwa kuwa anaishi na pamoja na familia ya Kiingereza katika jiji hilo na anafundishwa lugha hiyo na Sean Warren, ambaye pia anafanya kazi kwenye Academy ya klabu ya Manchester United.

Post a Comment

 
Top