0
Kiungo wa klabu ya Arsenal Aaron Ramsey amerejea mazoezini hapo jana (Jumatatu) akiwa tayari kabisa kwa mchezo wa michuano ya UEFA Champions League hii leo (Jumanne) dhidi ya timu ya Dinamo Zagreb kwenye dimba la Emirates.

Hizi zinaweza kuwa habari nzuri na zakuvutia masikioni mwa mashabiki wa klabu ya Arsenal kutokana na timu hiyo kukumbwa na kadhia kubwa ya wachezaji wake kuwa majeruhi.

Ikumbukwe kuwa kundi kubwa la wachezaji tegemezi wa klabu ya Arsenal kwa sasa wanasumbuliwa na majeruhi hali ambayo imeibua wasiwasi mkubwa miongoni mwa mashabiki wa klabu hiyo kutokana na timu hiyo kukabiliwa na michezo ya kufa na kupona ya michuano ya vilabu bingwa barani Ulaya.

Ziko pia taarifa zinazomuhusisha kiungo wa pembeni Alex Oxlade-Chamberlain kuwa nae yuko karibuni kurejea uwanjani na huenda akawa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kitakachojitupa ugani kwenye mchezo unaofuata wa ligi wa ugenini dhidi ya timu ya Norwich siku ya Jumaapili. 

Arsenal pia inatarajiwa kua na Theo Walcott na Thomas Rosicky kikosini kabla ya kipindi cha sherehe za Krismasi lakini pia mzee Wenger amesikika akidai kuwa anatarajiwa kufanya usajili wa mchezaji mmoja au wawili kwenye dirisha la usajiri la mwezi Januari.


Post a Comment

 
Top