Alexandre
Pato anatarajiwa kusaini mkataba wa kuitumikia klabu ya Liverpool mnamo mwezi wa January mwakani.
Kwa mujibu wa Raisi wa klabu ya Corinthians
ya nchini Brazil Robero de Andrade, ametanabahisha kuwa vilabu hivyo viwili vimekwishafanya makubaliano yote ta kimsingi yanayohusu mauzo ya mchezaji huyo.
Pato kwa sasa anacheza kwa mkopo kwenye klabu ya Sao Paulo akitokea kwenye klabu ya Corinthians ambapo mkataba wake unatarajia kumalizika mnamo mwezi Desemba mwaka huu na mshambuliaji huyo ameshathibitisha kuwa hayuko tayari kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa mkopo.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya AC Milan alilrejea nchini Brazil mnamo mwaka 2013 akitokea Italia amethibitisha kuwa anatarajia kukipiga nchini Uingereza au Hispania hapo mwakani bila ya kutaja timu atakayoitumikia.
Post a Comment