0
Mlinda mlango wa klabu ya Manchester United David de Gea amevunja ukimya na kudai kuwa anijiona kuwa mwenye bahati na furaha kwa ukwepo kwake ndani ya kikosi cha mashetani wekundu wa  Manchester United badala ya Real Madrid kama ambavyo ilikua inatarajiwa na wengi. 


Mlinda mlango huyo wa kikosi cha timu ya Taifa ya Hispania ambaye miezi michache iliyopita alikua ahamie Santiago Bernabeu dili lake lilishindikana nakika za mwisho za usajili kutokana na nyaraka zake za uhamisho kushindwa kufika kwa wakati. 


De Gea aliachwa kwenye kikosi cha kwanza cha mholanzi Louis Van Gaal kwenye kipindi chote cha mgogoro wake lakini sasa amerejea mahala pake na kuendelea kuwa mlinda mlango namba moja wa klabu hiyo mara baada ya kukubali kusaini kandarasi mpya itakayomfanya kubakia United kwa miaka minne zaidi.

Post a Comment

 
Top