KOCHA wa Simba Dylan Kerr, amesema itakuwa ngumu kumuuza kwa wapinzani wao Yanga beki wake wa kulia Hassan Ramadhani ‘Kessy’.
Kerr amesema kufanya hivyo itakuwa ni sawa na kumuuzia
adui yako silaha ambayo inaweza kukudhuru wewe mwenye na haoni sababu ya
kumuachilia mlinzi huyo kutokana na mchango aliokuwa nao kwenye kikosi
chake.
“Nibeki mdogo mwenye uwezo mkubwa najua kama mkataba wake unaelekea
kumalizika, chamsingi nitakachofanya kama kocha ni kuhakikisha uongozi
unamwongeza mkataba mpya ili aendelee kutusaidia,”amesema Kerr.
Muingereza huyo amesema Kess, amekuwa na msaada katika ushindi mwingi
wa Simba msimu huu kutokana na krosi zake pindi anapopanda mbele
kusaidia mashambulizi.
Post a Comment