KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ tayari
kimewasili Addis Ababa nchini Ethiopia leo alfajiri kikiwa na wachezaji
18 pamoja na viongozi tayari kwa mashindano ya Kombe la Chalenji
yatakayoanza kutimua vumbi kesho Jumamosi nchini humo.
Kilimanjaro Stars inayonolewa na Kocha Mkuu Abdallah Kibadeni, akisaidiwa na kocha msaidizi Juma Mgunda, imepangwa kundi A, ikiwa na wenyeji Ethiopia, Rwanda na Somalia.
Kilimanjaro Stars inayonolewa na Kocha Mkuu Abdallah Kibadeni, akisaidiwa na kocha msaidizi Juma Mgunda, imepangwa kundi A, ikiwa na wenyeji Ethiopia, Rwanda na Somalia.
Wengine ni viungo Himid Mao, Salum Abubakar, Jonas Mkude, Salum Telela na Said Ndemla, huku safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Malimi Busungu, Elias Maguri, Simon Msuva, Deus Kaseke na nahodha John Bocco.
Stars itacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Somalia siku ya Jumapili katika Uwanja wa Addis Ababa.
Post a Comment