TIMU ya JKT Ruvu, imeanza kujiimarisha kwa ajili ya
kufanya vizuri kwenye Ligi ya Vodacom baada ya kumsajili kiungo wa Stand
United Hassan Dilunga kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Kocha msaidizi wa JKT Ruvu, Mrage Kabange amesema, kuwa
wamemtaka kiungo huyo kwa ajili ya kuimarisha eneo la kiungo ambalo
limeonyesha mapungufu katika mechi za awali kitu kilichochangia waanze
vibaya ligi ya msimu huu.
“Tunaimani anaweza kufanya vizuri kwasababu tumekuwa tukimfuatilia
tangu akiwa Yanga anauwezo mkubwa na ndiyo sababu
tukampendekeza,”amesema Kabange.
Kikosi cha JKT Ruvu kimeshindwa kufanya vizuri kwenye michezo yake ya
ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu huu ikiwa imeshinda mchezo
mmoja pekee kati ya 10 huku ikienda sare mara mbili na kupoteza michezo
saba.
Kikosi hicho kimeamua kujipanga kwa kufanya usajili katika nafasi kadhaa
kuhakikisha kinafanya vizuri na kurejea kwenye nafasi nzuri kwenye
msimamo wa ligi kuu Tanzania bara kwani kwa sasa wako nafasi ya 14 kati
ya timu 16.
Post a Comment