0
kikosi kamili sha Ryan Giggs.
Mchezaji wa zamni wa klabu ya Manchester United amabaye kwa sasa ni kocha msaidizi wa klabu hiyo Ryan Giggs ametaja wachezaji 11 anaowadhania kuwa ni hatari zaidi kuwahi kutoke ndani ya klabu hiyo juku akimnyima kabisa nafasi George Best na Steve Bruce katika kikosi hicho. 

Aidha licha ya uhodari aliokuwa nao mchezaji huyo enzi zake katika usakataji wa kabumbu pia mchezaji huyo amejinyima nafasi yeye mwenyewe kwenye kikosi hicho licha ya kiwango cha juu cha uchezaji na mafanikio makubwa aliyoyapata akiwa na timu hiyo katika karia yake ya uchezaji.Kikosi kamili cha kocha huyo ni hiki hapa.

1. Peter Schmeichel. (Mlinda mlango)

Peter Schmeichel (kushoto) na  Giggs wakisherehekea ubingwa wa Ulaya wa msimu wa mwaka 1998-1999.
2. Gary Neville. (Mlinzi wa kulia)

Giggs (Katikati) akiwa na Scholes (kushoto) na Neville (kulia) wakiwa na tuzo walizozawadiwa.
3. Denis Irwin. (Mlinzi wa kushoto)

Denis Irwin (kushoto) ambaye alidumu United kwa miaka 12 akiwa na Ryan Giggs.
4. Jaap Stam. (Mlinzi wa kati)
  
Jaap Stam (kushoto) akimpongeza Giggs.
5. Rio Ferdinand. (Mlinzi wa kati)

Rio Ferdinand (kushoto) na Giggs wakifurahia mafanikio waliyoyapata pamoja ndani ya Manchester United, ikiwemo kushinda mataji sita tofautitofauti.
6. Roy Keane. (Kiungo mkabaji)

Roy Keane katikati akiwa pamoja na Giggs (kulia) na Beckham (kushoto) anatajwa na Giggs kuwa ndiye nahodha bora kabisa yeye kuwahi kufanya nae kazi katika maisha yake yote ya soka.
7. David Beckham. (Kiungo mshambuliaji upande wa kulia)

David Beckham (wa pili kulia) anatajwa na Giggs kuwa ndiye mpiga krosi bora kuwahi kutokea duniani katika maisha yote ya mpira wa miguu ambayo Giggs amekwisha yaishi na anayoendelea kuishi.
8. Paul Scholes. (Kiungo mshambuliaji)

Poul Scholes (kushoto) anatwjwa kuwa ni kiungo bora kabisa kuwawi kucheza pamoja na Giggs.
9. Eric Cantona. (Mshambuliaji)

Cantona (kulia) anatajwa na Giggs kuwa ni mtambo wa kufunga na kutengeneza mabao ambao ushawahi kufanya kazi hiyo ndani ya United.
10. Wayne Rooney. (Mshambuliaji)

Giggs alicheza pamoja na mshambuliaji Wayne Rooney (katikati) mpaka kustaafu kwake, na wawili hao bado wanafanya kazi pamoja mpaka sasa Giggs akiwa kama kocha msaidizi.
11. Cristiano Ronaldo. (Kiungo mshambuliaji upande wa kushoto)

Cristiano Ronaldo (katikati) aliitumia klabu ya Manchester United kama njia ya yeye kujitangaza kuwa mchezaji bora kabisa ulimwenguni.

Post a Comment

 
Top