Wapinzani wakuu kwenye soka la Afrika ya Mashariki timu za mataifa ya Kenya (Harambee Stars) na Uganda (The Cranes) zinatarajia kujitupa ugani jioni hii kwenye mchezo wa kundi B kwenye uwanja wa Taifa wa Ethiophia uliopo katika jiji la
Addis Ababa.
Takwimu zinaonesha kuwa tangu mwaka 2004 Uganda amefanikiwa kumfunga Kenya takribani mara 6 na kutoka sare mara tatu katika mara zote 9 ambazo timu hizi zimekutana katika michuano mbalimbali.
Halikadhalika takwimu zinaonesha kuwa sasa ni takribani miaka 11 Harambee Stars haijapata matokeo ya ushindi dhidi ya The Cranes.
Uganda ndio timu pekee kutoka ukanda wa Afrika ya mashariki ambayo imefanikiwa kuingia kwenye hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya kufuzu kwa michuano ya kombe la Dunia ya mwaka 2018 baada ya kuwavurumisha Togo kwenye mechi ya mtoano wiki moja iliyopita.
Mkufunzi Bobby Williamson ambaye ameshinda mara nne ubingwa wa michuano ya Cecafa akiwa na timu ya Taifa ya Uganda kwa sasa anakinoa kikosi cha
Harambee Satrs anakwenda kuvaana uso kwa uso na mrithi wake Mserbia Sredojevic “Micho” Milutin.
Vikosi vinatarajiwa kuwa hivi kuelekea mchezo wa leo;
Kenya: Boniface Oluoch, Noah Abich, Omar Mbongi, David Owino, Haron
Shakava, Anthony Akumu, Collins Okoth, Clifton Miheso, Kevin Kimani,
Michael Olunga and Allan Wanga.
Uganda: James Walitho, Dennis Okot, Joseph Ochaya, Murushid Jjuko,
Joseph Nsubuga, Muzamiru Mutyaba, Kizito Keziron, Faruku Miya, Erisa
Ssekisambu, Ceaser Okhuti and Frank Kalanda.
Post a Comment