Simba SC imesema mpango wake wa kumsajili
mshambuliaji wa Burundi, Laudit Mavugo unakwamishwa na klabu ya Vital’O
ambayo haitaki kutoa ushirikiano.
Simba wanaonekana wamedhamiria kumsajili mshambuliaji wa Burundi,
Laudit Mavugo lakini inaonekana mpango huo unakwamishwa na klabu ya
Vital’O ambayo haitaki kutoa ushirikiano.
Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva amedai kwamba wanafanya jitihada za kuwapata viongozi wa Vital’O ili wazungumzie suala la Mavugo, lakini hawapati ushirikiano wao.
Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva amedai kwamba wanafanya jitihada za kuwapata viongozi wa Vital’O ili wazungumzie suala la Mavugo, lakini hawapati ushirikiano wao.
“Kuna watu wanasema Mavugo kamaliza Mkataba Vital’O, lakini habari
kutoka Vital’O zinasema bado ana Mkataba hadi mwishoni mwa msimu. Sasa
inatuchanganya kwa kweli,” alisema Bw. Aveva.
Hata hivyo, Aveva amesema dhamira bado ni kumsajili Mavugo na wanaendelea na jitihada kuhakikisha wanafanikiwa.
Amesema iwapo watamkosa Mavugo, basi watamgeukia Mrundi mwingine, Kelvin Ndayisenga ambaye yeye iko wazi hana Mkataba.
Aidha, Aveva amethibitisha klabu yake kuwaacha Simon Sserunkuma na
Msenegali, Abdoulaye Pape N’daw na kumrejesha Mkenya, Paul Kiongera.
Kuhusu Mganda mwingine, Brian Majwega ambaye jana alianza mazoezi na
Simba SC, Aveva amesema winga huyo ameomba kufanya mazoezi na timu hiyo
wakati huu ambao ana mgogoro na klabu yake, Azam FC.
Pamoja na hayo, Aveva amesema Kamati ya Usajili ya klabu yake, chini
ya Mwenyekiti, Zacharia Hans Poppe imepewa jukumu la kusajili mabeki
wawili wa kati.
“Kwa ujumla ripoti ya benchi la Ufundi imependekeza kusajiliwa mabeki
wawili wa kati, kiungo wa pembeni mmoja na washambuliaji wawili,”
alimalizia.
Post a Comment