Klabu za Chelsea na West Ham
zimelimwa faini na shirikisho la soka nchini Uingereza FA kwa kushindwa kuwaongoza vyema wachezaji wao kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza uliozikutanisha timu hizo.
Vijana wa Jose Mourinho wamelimwa faini ya paundi 50,000 wakati wagonga nyundo wa jiji la London wao watalazimika kulipa kiasi cha paundi 40,000.
Kwenye mchezo wao uliopigwa kwenye dimba la Upton Park ambao ulishuhudia klabu ya Chelsea ikiangukia pua kwa kupigwa jumla ya magoli 2-1 mchezaji wa Chelsea Nemanja Matic alizawadiwa kadi nyekundu kwenye mchezo huo.
Post a Comment