0

Mpira rasmi kwajili ya michuano ya Ulaya (Euro) ya mwaka 2016 imewekwa hadharani na kampuni ya Adidas ambao wamepewa jukumu la kutengeneza mipira hiyo.


Mipira hiyo imepewa jina la kifaransa Beau Jeu, ambayo kwa kingereza linamaanisha "the beautiful game", imeichukua kampuni ya Adidas takribani miezi 18 kuitengeneza mipira hiyo.


Taarifa kutoka kwenye kampuni ya Adidas inadai kwamba mpira huo kwa kiasi fulani inafanana sana na mipira iliyotumika kwenye fainali za kombe la Dunia kule nchini Brazil mwaka 2014 iliyopewa jina la Brazuka.

Kwa mujibu wa msemaji wa kampuni ya Adidas kampuni hiyo inajiandaa kuikabidhi UEFA mipira ya mashindano hayo mnamo mwezi Novemba na hivyo kuwapa wachezaji takribani miezi sita ya kuifanyia mazoezi na kuizoea mipira hiyo kabla ya mashindano hayo kuanza mnamo mwezi Juni mwakani. 


Post a Comment

 
Top