0
TAIFA Stars wameondolewa kwenye mbio za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 zitakazofanyika nchini Russia lakini wana adhabu ya kulipa Dola 5000 sawa na Sh 10 milioni kwasasa.

Faini hiyo ni kwa ajili ya kadi za njano walizopewa wachezaji wao saba kwenye mechi ya ugenini walipocheza na Algeria wiki hii ikiwa ni mechi ya marudiano ambapo walifungwa mabao 7-0.

Wachezaji waliopewa kaadi za njano siku ya mechi hiyo ni Nadir Haroub 'Canavaro', Haji Mwinyi, Himid Mao, Farid Musa, Kevin Yondani,  Aishi Manula, Mudathir Yahya aliyepewa kadi mbili za njano na moja nyekundu.

Kocha Mkuu wa Stars, Boniface Mkwassa amesema kuwa wamefungwa mabao mengi ambayo ni kipigo chake cha kwanza tangu aanze kuwa kocha kwa miaka 25 sasa lakini wamepata adhabu hiyo ambayo kikanuni ni lazima walipe fedha hizo Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

"Hiki ni kipigo kikubwa, tumepata kadi nyingi za njano ugenini ambapo kanuni ya mashindani hayo ukiwa na kadi nyingi za njano ambazo ni kuanzia tano ugenini ni lazima upigwe faini ya dola 5000, sheria hiyo iko wazi," alisema Mkwassa.

Post a Comment

 
Top