0

Klabu ya PSG ya nchini Ufaransa imesema kuwa itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa inamshawishi mshambuliaji wa klabu nya Real Madrid Cristiano Ronaldo atue kwenye klabu hiyo kwa kumfanya kuwa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi ulimwenguni.

Ronaldo pia anawaniwa kwa udi na uvumba na klabu yake ya zamani ya Manchester United ambayo mabosi wake wanaonekana kutaka kumrejesha tena kwa mara ya pili klabuni hapo mshambuliaji huyo machachari dimbani raia wa Ureno kutoka klabu ya Real Madrid.

Klabu hiyo ya nchini Ufaransa imesema kuwa wako tayari kumpatia ronaldo mzigo wa paundi 500,000 kwa wiki na hii ikiwa baada ya kutoa kodi na makato mengine muhimu ya kisheria anayostahili kulipa mchezaji wa kimataifa anayecheza soka la kimataifa kwenye ligi kuu ya soka ya nchini Ufaransa.

Wakati vilabu hivi viwili vyenye nguvu ya fedha barani Ulaya vikionekana kupigana vikumbo kuwania saini ya mshambuliaji huyo tayari wakala wa mchezaji huyo Jorge Mendes amethibitisha kuwa haoni uwezekano wa mshambuliaji huyo kuondoka ndani ya klabu ya Real Madridi kwa sasa japo alikiri kuwa lolote laweza kutokea.

Post a Comment

 
Top