0


Antonio Valencia ametuma picha akiwaonesha dole dumba mashabiki wake na wa Manchester United ikiashiria kuwa mambo yako safi kabisa mara baada ya kufanyia opasuaji wa mguu wake wa kushoto.


Winga huyo mwenye kasi kubwa raia wa Equado alitolewa kabla ya muda wa mwisho wa mchezo uliomalizika kwa sare ya kutokufungana baina ya klabu yake ya Manchester United na mahasimu wao wakubwa  Manchester City mwezi uliopita.


Valencia ametuma picha kwenye mtandao wa Tweeter inayomuonesha akiwa kitandani na sambamba na picha hiyo ameandika 'Namshukuru Mungu upasuaji wangu umekwenda sawa kwasasa ninafikiria jinsi nitakavyoweza kupona kwa haraka na kurejea kwenye majukumu yangu ya kawaida.'



Valencia kwakiasi kikubwa amekuwa anatumika kama mlinzi wa pembeni na Mholanzi Louis van Gaal badala ya nafasi yake ya asili aliyozoea. 

Kuumia kwa Valencia kumethibitisha msemo wa waswahili kufa kufaana kwani maumivu hayo yamepelekea kinda la umri wa miaka 18 Mkameroon Borthwick-Jackson kukaa kwenye benchi la klabu ya United na kupata nafasi ya kumsaidia Marcos Rojo kwa robo saa kwenye mchezo ambao ilishuhudiwa klabu ya United ikiibuka na ushindi wa magoli 2:0 dhidi ya West Brom siku ya Jumaapili.



Post a Comment

 
Top