Kiungo wa klabu ya Arsenal mfaransa Francis Coquelin anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu.
Kiungo huyo kijana mwenye umri wa miaka 24 wa klabu ya Arsena anaungana na kiungo mwenzake Mikel Arteta,kwenye orodha ya msululu mrefu wa majeruhi ndani ya klabu ya Arsenal.
Coquelin alimpisha Muhispania Arteta dakika ya 14 tu ya mchezo ambao klabu ya Arsenal iliangukia pua kwenye dimba la Hawthorns, ambaye pia baadae alitoka nje mnamo dakika ya nne tu ya kipindi cha pili cha mchezo.
Coquelin amefanyiwa vipimo vya afya siku ya jumaapili na Meneja wa klabu yake Mfaransa Arsene Wenger
hapo jana (Jumaatatu) amethibitisha kuwa mfaransa huyo atakua nje ya uwanja mpaka mwishoni mwa mwezi Januari akiuguza jeraha lake siku ambayo Arsenal watakua wakikipiga dhidi ya Chelsea.
Orodha ya wachezaji wengine wa Arsenal waliomajeruhi na tarehe zao watakazorejea dimbani ni;
Post a Comment