0
Nahodha wa zamani wa klabu ya Liverpool Muingereza Steven Gerrard anatarajiwa kuvaa tena uzi wa klabu yake hiyo ya zamani hapo mwakani ambapo maligendari wa klabu ya Liverpool watakapowavaa maligendari wenzao wa soka wa nchini Australia kwenye mji wa Sydney hapo Januari mwakani.

Nahodha huyo wa zamani wa Liverpool atawaongoza maveterani wenzake kama Jamie Carragher, Ian Rush, Dietmar Hamann na Luis Garcia kwenye mchezo huo unaotarajiwa kufanyika kwenye dimba la ANZ Stadium januari 7 mwakani ambapo meneja wa zamani wa timu hiyo Gerrard Houllier ataliongoza benchi la ufundi.


Post a Comment

 
Top