Klabu ya soka ya Manchester United ya nchini Uingereza imetangaza ongezeko la mapato yake kwa asilimia 39 katika robo ya kwanza ya mwaka. Kwa mujibu wa mabosi wa klabu hiyo.
Mapato hayo yameongezeka kutokana na timu hiyo kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya na pia mauzo ya jezi mpya zilizodizainiwa na kamapuni ya Adidas ya Ujerumani.
United kwa sasa iko katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza ilishindwa kufuzu kwaajili ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya vilabu barani Ulaya kwenye msimu uliopita mara baada ya kumaliza ikiwa katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa EPL kwenye msimu wa 2013/14.
Klabu hii inayomilikiwa na familia ya bilionea wa Kimarekani ya Glazer imetajwa kuwa mapato yake yameongezeka mpaka kufikia paundi 123.6 milloni (Dola 187.60 milioni) katika miezi mitatu iliyopita mpaka kufikia September 30, ambapo kwa mwaka uliopita kwa kipindi kama hicho ilikua paundi za Uingereza 88.7
Post a Comment