Mbeya City inatarajia kumpa mkataba wa mwaka mmoja na
nusu kipa wake mkongwe Juma Kaseja Juma, ambaye mkataba wake wa sasa
unakwisha mwezi ujao.
Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, amesema wameridhishwa na utendaji wa kipa huyo mkongwe na wapo katika
mazungumzo ya kuona uwezekano wa kumuongezea mkataba.
“Tupo kwenye mazungumzo na ninaamini tutaelewana kwa sababu tumeishi
na Kaseja vizuri na hatujawahi kupishana nasi kama waajiri tumeridhishwa
na utendaji wake,”amesema Kimbe.
Katibu huyo amesema wamepanga kusajili wachezaji watatu kwenye
dirisha dogo la usajili na Kaseja atakuwa mchezaji wa nne na mipango yao
ni kuhakikisha timu hiyo inazinduka na kufanya vizuri kama ilivyokuwa
msimu uliopita.
Mbeya City haijafanya vizuri na imepoteza michezo mitano tangu kuanza
kwa msimu huu na Kaseja aliyejiunga na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu
ametoa mchango katika ushindi wa mechi tatu walizoshinda.
Post a Comment