MABAO yaliyofungwa na Gary Cahill, Willian, Oscar na Kurt Zouma yameipa Chelsea pointi tatu muhimu kufuatia ushindi wake wa 4-0 dhidi ya Maccabi Tel Aviv katika mchezo wa kundi wa Ligi ya Mabingwa.
Wakati Chelsea ikipata ushindi huo wa magoli 4-0, Porto
iliyokuwa inaongoza kundi G, imeshushwa hadi nafasi ya pili baada ya
kufungwa 2-0 na Dynamo Kyiv.
Porto na Chelsea zote zina pointi 10, lakini mabingwa hao wa England wanaogoza kundi G kwa wastani mzuri wa magoli.
Porto na Chelsea zote zina pointi 10, lakini mabingwa hao wa England wanaogoza kundi G kwa wastani mzuri wa magoli.
Dynamo Kyiv ni ya tatu kwa pointi
zake 8 na kufanya nafasi ya kufuzu kwenda 16 bora iwe wazi kwa timu zote
tatu za juu kutegemea na matokeo yao ya mwisho yatakavyokuwa Disemba 9
ambapo Chelsea itaumana na Porto na huku Maccabi Tel Aviv wakiwa uso kwa
uso na Dynamo Kyiv.
Post a Comment